Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:145

6:145
قل لا اجد في ما اوحي الي محرما على طاعم يطعمه الا ان يكون ميتة او دما مسفوحا او لحم خنزير فانه رجس او فسقا اهل لغير الله به فمن اضطر غير باغ ولا عاد فان ربك غفور رحيم ١٤٥
قُل لَّآ أَجِدُ فِى مَآ أُوحِىَ إِلَىَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍۢ يَطْعَمُهُۥٓ إِلَّآ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًۭا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍۢ فَإِنَّهُۥ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ ۚ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍۢ وَلَا عَادٍۢ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌۭ رَّحِيمٌۭ ١٤٥
قُل
لَّآ
أَجِدُ
فِي
مَآ
أُوحِيَ
إِلَيَّ
مُحَرَّمًا
عَلَىٰ
طَاعِمٖ
يَطۡعَمُهُۥٓ
إِلَّآ
أَن
يَكُونَ
مَيۡتَةً
أَوۡ
دَمٗا
مَّسۡفُوحًا
أَوۡ
لَحۡمَ
خِنزِيرٖ
فَإِنَّهُۥ
رِجۡسٌ
أَوۡ
فِسۡقًا
أُهِلَّ
لِغَيۡرِ
ٱللَّهِ
بِهِۦۚ
فَمَنِ
ٱضۡطُرَّ
غَيۡرَ
بَاغٖ
وَلَا
عَادٖ
فَإِنَّ
رَبَّكَ
غَفُورٞ
رَّحِيمٞ
١٤٥
Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, mimi sipati, kati ya yale aliyoniletea wahyi Mwenyezi Mungu, kitu kilicho haramu kwa mwenye kukila, kati ya vile mnavyovitaja kwamba vimeharamishwa miongoni mwa wanyama howa, isipokuwa awe amekufa bila kuchinjwa, au ni damu itiririkayo, au iwe ni nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni najisi, au akawa ni mnyama ambaye kuchinjwa kwake kumetoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama akiwa mnyama aliyechinjwa ametajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kuchinjwa. Basi mwenye kulazimika kula chochote kati ya hizo zilizoharamishwa kwa dharura ya njaa kali, pasi na kutaka kujifurahisha wala kukiuka mpaka wa dharura, hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni mwenye kumsamehe, ni mwenye huruma naye. Na hakika imethibiti, baadaye, kwa mafundisho ya Mtume kuwa ni haramu kula kila mnyama mwitu anayewinda kwa kutumia meno, kila ndege anayewinda kwa kutumia kucha, punda na mbwa.