Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:151

6:151
۞ قل تعالوا اتل ما حرم ربكم عليكم الا تشركوا به شييا وبالوالدين احسانا ولا تقتلوا اولادكم من املاق نحن نرزقكم واياهم ولا تقربوا الفواحش ما ظهر منها وما بطن ولا تقتلوا النفس التي حرم الله الا بالحق ذالكم وصاكم به لعلكم تعقلون ١٥١
۞ قُلْ تَعَالَوْا۟ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا۟ بِهِۦ شَيْـًۭٔا ۖ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًۭا ۖ وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَوْلَـٰدَكُم مِّنْ إِمْلَـٰقٍۢ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا۟ ٱلْفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا۟ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ١٥١
۞ قُلۡ
تَعَالَوۡاْ
أَتۡلُ
مَا
حَرَّمَ
رَبُّكُمۡ
عَلَيۡكُمۡۖ
أَلَّا
تُشۡرِكُواْ
بِهِۦ
شَيۡـٔٗاۖ
وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ
إِحۡسَٰنٗاۖ
وَلَا
تَقۡتُلُوٓاْ
أَوۡلَٰدَكُم
مِّنۡ
إِمۡلَٰقٖ
نَّحۡنُ
نَرۡزُقُكُمۡ
وَإِيَّاهُمۡۖ
وَلَا
تَقۡرَبُواْ
ٱلۡفَوَٰحِشَ
مَا
ظَهَرَ
مِنۡهَا
وَمَا
بَطَنَۖ
وَلَا
تَقۡتُلُواْ
ٱلنَّفۡسَ
ٱلَّتِي
حَرَّمَ
ٱللَّهُ
إِلَّا
بِٱلۡحَقِّۚ
ذَٰلِكُمۡ
وَصَّىٰكُم
بِهِۦ
لَعَلَّكُمۡ
تَعۡقِلُونَ
١٥١
Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Waambie, ewe Mtume, «Njooni niwasomee Yale Aliyoyaharamishia Mwenyezi Mungu: Msishirikishe pamoja na Mwenyezi Mungu kitu chochote, miongoni mwa viumbe Vyake katika kumuabudu Yeye; bali zielekezeni aina zote za ibada Kwake Yeye Peke Yake, kama kucha, kutaraji, kuomba na megineyo. Muwafanyie wema wazazi wawili kwa kuwasaidia, kuwaombea Mungu na mengineyo ya wema kama hayo Msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara uliowshukia, kwani Mwenyezi Mungu Anawaruzuku nyinyi na wao. Wala msiyasongelee madhambi makubwa yaliyo wazi na yaliyofichika. Na msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuawa, isipokuwa kwa njia ya haki, nayo ni kuchukuliwa kisasi kwa aliyeua, au kwa uzinifu baada ya kuoa au kuolewa, au kuacha Uislamu. Hayo yaliyotajwa ni miongoni mwa yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewkataza nayo na Akawapa maagizo muyaepuke na ni miongoni mwa yale Aliyowaamrisha nyinyi kwayo. Amweausia nayo Mola wenu ili mupate kuyaitia akilini maamrisho Yake na Makatazo Yake.