Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenye kukutana na Mola wake, Siku ya Kiyama, akiwa na jema moja miongoni mwa matendo mazuri, atapata mema mfano wake mara kumi. Na mwenye kukutana na Mola wake akiwa ana ovu moja, hatateswa isipokuwa kadiri ya mfano wa ovu hilo, na wao hawatadhulumiwa hata kiasi cha uzito wa chungu mdogo.