Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala wao hawatambui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na washirikina hawa wanawakataza watu kumfuata Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kumsikiliza, na wao wenyewe wanajiepusha naye. Na wao hawamuangamizi yoyote, kwa kuzuia kwao njia ya Mwenyezi Mungu isifuatwe, isipokuwa nafsi zao wenyewe, na wao hawatambui kuwa wajishughulisha na mambo ya kuzitia kwenye maangamivu.