Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:27

6:27
ولو ترى اذ وقفوا على النار فقالوا يا ليتنا نرد ولا نكذب بايات ربنا ونكون من المومنين ٢٧
وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ وُقِفُوا۟ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُوا۟ يَـٰلَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٢٧
وَلَوۡ
تَرَىٰٓ
إِذۡ
وُقِفُواْ
عَلَى
ٱلنَّارِ
فَقَالُواْ
يَٰلَيۡتَنَا
نُرَدُّ
وَلَا
نُكَذِّبَ
بِـَٔايَٰتِ
رَبِّنَا
وَنَكُونَ
مِنَ
ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
٢٧
Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na lau utawaona, ewe Mtume, washirikina hawa Siku ya Kiyama, utaona jambo kubwa, nalo ni wakati wao watakapofungwa juu ya Moto, na watakaposhuhudia yaliyomo humo miongoni mwa minyororo na pingu, na kujionea kwa macho yao mambo makubwa hayo na vituko hivyo. Hapo watasema, «Twatamani turudishwe kwenye maisha ya kilimwengu, tupate kuziamini aya za Mwenyezi Mungu na tuzitumie na tuwe ni miongoni mwa Waumini.»