Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:3

6:3
وهو الله في السماوات وفي الارض يعلم سركم وجهركم ويعلم ما تكسبون ٣
وَهُوَ ٱللَّهُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَفِى ٱلْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ٣
وَهُوَ
ٱللَّهُ
فِي
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَفِي
ٱلۡأَرۡضِ
يَعۡلَمُ
سِرَّكُمۡ
وَجَهۡرَكُمۡ
وَيَعۡلَمُ
مَا
تَكۡسِبُونَ
٣
Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini. Anajua ya ndani yenu na ya nje yenu. Na anajua mnayo yachuma. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki mbinguni na ardhini. Na miongoni mwa dalili za uungu wake ni kwamba Yeye Anayajua yote mnayoyaficha, enyi watu, na mnayoyadhihirisha na Anayajua matendo yenu yote, mazuri na mabaya. Na kwa ajili hii, Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye Mola Anayestahiki kuabudiwa.