Na maisha ya dunia si chochte ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Maisha ya kilimwengu hayakuwa, katika wingi wa hali zake, isipokuwa ni udanganyifu na ubatilifu. Na matendo mema, kwa kutengeneza nyumba ya Akhera, ndiyo bora kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu, wakajikinga na adhabu Yake kwa kumtii na kujiepusha na mambo ya kumuasi. Kwani hamuelewi, enyi washirikina mlioghurika na pambo la uhai wa kilimwengu, mukayatanguliza yanayosalia mbele ya yanayomalizika?