Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika sisi tunajua kwamba msimamo wa kaumu zako wa kukukanusha waziwazi unakutia huzuni moyoni mwako. Basi subiri na ujitulize. Kwani wao hawakukanushi wewe kutoka ndani ya roho zao; wao waamini ukweli wako, lakini wao kwa udhalimu na uadui walionao, wanazikataa hoja zilizo wazi zinazoonyesha ukweli wako, ndipo wakakufanya mrongo kwa yale uliyokuja nayo.