Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:35

6:35
وان كان كبر عليك اعراضهم فان استطعت ان تبتغي نفقا في الارض او سلما في السماء فتاتيهم باية ولو شاء الله لجمعهم على الهدى فلا تكونن من الجاهلين ٣٥
وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ ٱسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِىَ نَفَقًۭا فِى ٱلْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًۭا فِى ٱلسَّمَآءِ فَتَأْتِيَهُم بِـَٔايَةٍۢ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى ٱلْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ ٣٥
وَإِن
كَانَ
كَبُرَ
عَلَيۡكَ
إِعۡرَاضُهُمۡ
فَإِنِ
ٱسۡتَطَعۡتَ
أَن
تَبۡتَغِيَ
نَفَقٗا
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
أَوۡ
سُلَّمٗا
فِي
ٱلسَّمَآءِ
فَتَأۡتِيَهُم
بِـَٔايَةٖۚ
وَلَوۡ
شَآءَ
ٱللَّهُ
لَجَمَعَهُمۡ
عَلَى
ٱلۡهُدَىٰۚ
فَلَا
تَكُونَنَّ
مِنَ
ٱلۡجَٰهِلِينَ
٣٥
Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na iwapo umekuwa ni mzito kwako, ewe Muhammad, upinzani wa hawa washirikina na kujiepusha kwao kukubali ulinganizi wako, basi ukiweza kujifanyia mapito ndani ya ardhi, au ngazi ya kupandia mbinguni ili uwaletee alama na dalili ya usahihi wa maneno yako, zisizokuwa hizi tulizokuletea, fanya hivyo. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka kuwakusanya kwenye uongofu ambao nyinyi munao na kuwaongoza kwenye Imani, Angalifanya hivyo. Lakini Hakulitaka hilo, kwa hekima Anayoijua Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake. Basi, usiwe kabisa ni miongoni mwa wale wajinga ambao huzuni zao zilizidi na wakawa na majonzi mpaka hayo yakawapelekea kwenye babaiko kubwa.