Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Nipeni habari, ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ulimwenguni, au ikawajia saa ya nyinyi kufufuliwa, je, mutamuomba hapo asiyekuwa Mwenyezi Mungu awaondolee shida iliyowakumba, iwapo nyinyi ni wakweli kwamba waungu wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wanawanufaisha au kuwadhuru?»