Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:53

6:53
وكذالك فتنا بعضهم ببعض ليقولوا اهاولاء من الله عليهم من بيننا اليس الله باعلم بالشاكرين ٥٣
وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍۢ لِّيَقُولُوٓا۟ أَهَـٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنۢ بَيْنِنَآ ۗ أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَعْلَمَ بِٱلشَّـٰكِرِينَ ٥٣
وَكَذَٰلِكَ
فَتَنَّا
بَعۡضَهُم
بِبَعۡضٖ
لِّيَقُولُوٓاْ
أَهَٰٓؤُلَآءِ
مَنَّ
ٱللَّهُ
عَلَيۡهِم
مِّنۢ
بَيۡنِنَآۗ
أَلَيۡسَ
ٱللَّهُ
بِأَعۡلَمَ
بِٱلشَّٰكِرِينَ
٥٣
Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao shukuru? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hivyo basi Mwenyezi Mungu Amewapa mtihani waja Wake kwa kutafautiana mafungu yao ya riziki na umbo, Akawafanya baadhi yao matajiri na wengine maskini, baadhi yao wenye nguvu na wengine madhaifu Na Akawafanya baadhi yao ni wahitaji wa wengine ili kuwajaribu kwa hilo, wapate makafiri matajiri kusema, «Ni madhaifu hawa, miongoni mwetu, Mwenyezi Mungu Amewapa neema ya Uislamu?» Kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, si Mjuzi zaidi wa wanaoshukuru neema Yake Akawaafikia kwenye uongofu wa dini Yake?