Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ibrāhīm alipouona mwezi umechomoza alisema kuwaambia watu wake kwa njia ya kumvuta mtesi, «Huu ni mola wangu.» Ulipozama, alisema, akiwa ahitajia uongofu wa Mola wake, «Asiponiongoza Mola wangu kwenye usawa juu ya kumpwekesha Yeye nitakuwa ni miongoni mwa watu waliopotea njia ya sawa kwa kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.