Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hoja hiyo ambayo Ibrāhīm, amani imshukiye, aliwahoji nayo watu wake ndiyo hoja yetu tuliyomuongoza nayo mpaka hoja yao ikakatika. Tunamtukuza daraja tunayemtaka, miongoni mwa waja wetu, ulimwenguni na Akhera, Hakika Mola wako ni Mwenye hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake, ni Mjuzi kuhusu wao.