Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:84

6:84
ووهبنا له اسحاق ويعقوب كلا هدينا ونوحا هدينا من قبل ومن ذريته داوود وسليمان وايوب ويوسف وموسى وهارون وكذالك نجزي المحسنين ٨٤
وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ٨٤
وَوَهَبۡنَا
لَهُۥٓ
إِسۡحَٰقَ
وَيَعۡقُوبَۚ
كُلًّا
هَدَيۡنَاۚ
وَنُوحًا
هَدَيۡنَا
مِن
قَبۡلُۖ
وَمِن
ذُرِّيَّتِهِۦ
دَاوُۥدَ
وَسُلَيۡمَٰنَ
وَأَيُّوبَ
وَيُوسُفَ
وَمُوسَىٰ
وَهَٰرُونَۚ
وَكَذَٰلِكَ
نَجۡزِي
ٱلۡمُحۡسِنِينَ
٨٤
Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tulimneemesha Ibrāhīm, amani imshukiye, kwa kumruzuku Is’ḥāq kuwa mtoto wake na Ya‘qūb kuwa mjukuu. Na wote wawili tuliwaongoza kwenye njia ya uongofu. Pia tulimuongoza Nūḥ kwenye haki, kabla ya Ibrāhīm na Isḥāq na Ya’qūb. Na pia tuliwaongoza kwenye haki, kati ya kizazi cha Nūḥ, Dāwūd, Sulaimān, Ayyūb, Yūsuf, Mūsā na Hārūn, amani iwashukie. Na kama tulivyowajazi Manabii hawa kwa wema wao, ndivyo tunavyomjazi kila mwema.