Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa kwenye Njia iliyo nyooka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na pia tuliwaongoza kwenye haki tuliowataka kuwaongoza kati ya wazazi wa hawa, watoto wao na ndugu zao. Na tuliwateua wao wafuate Dini yetu na wafikishe ujumbe wetu kwa wale tuliowatuma kwao. Na tuliwaonesha njia sahihi, isiyopotoka, nayo ni ile ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kumwepusha na mambo ya kumshirkisha..