Na kama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka tungeli mfanya kama binaadamu, na tungeli watilia matatizo yale wanayo yatatiza wao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na lau kama tulimfanya mtume aliyeteremshwa kwao ni Malaika, kwani hawakukinai na Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, tungalimfanya Malaika huyo kwenye sura za mwanadamu, ili waweze kumsikia na kusema naye. Kwani haimkiniki kwao kumuona Malaika katika sura zake za kimalaika. Na lau Malaika aliwajia kwa sura za mtu, jambo hilo lingaliwafanya wachanganyikiwe kama lilivyowafanya wachanganyikiwe jambo la Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.