Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:90

6:90
اولايك الذين هدى الله فبهداهم اقتده قل لا اسالكم عليه اجرا ان هو الا ذكرى للعالمين ٩٠
أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُ ۖ فَبِهُدَىٰهُمُ ٱقْتَدِهْ ۗ قُل لَّآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَـٰلَمِينَ ٩٠
أُوْلَٰٓئِكَ
ٱلَّذِينَ
هَدَى
ٱللَّهُۖ
فَبِهُدَىٰهُمُ
ٱقۡتَدِهۡۗ
قُل
لَّآ
أَسۡـَٔلُكُمۡ
عَلَيۡهِ
أَجۡرًاۖ
إِنۡ
هُوَ
إِلَّا
ذِكۡرَىٰ
لِلۡعَٰلَمِينَ
٩٠
Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Manabii hao waliotajwa ndio ambao Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewaongoza kwenye dini Yake ya haki. Basi fuata uongofu wao, ewe Muhammad, na andama njia yao. Waambie washirikina, «Mimi sitaki kutoka kwenu, kwa kufikisha Uislamu, badala ya ulimwengu. Malipo yangu yako kwa Mwenyezi Mungu. Na Uislamu ni kuita watu wote kwenye njia iliyolingana sawa na ni ukumbusho kwenu na kwa kila aliyekuwa kama nyinyi, kati ya wale wanaoendelea kwenye batili; huenda nyinyi mkawaidhika nao mkanufaika.