Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:94

6:94
ولقد جيتمونا فرادى كما خلقناكم اول مرة وتركتم ما خولناكم وراء ظهوركم وما نرى معكم شفعاءكم الذين زعمتم انهم فيكم شركاء لقد تقطع بينكم وضل عنكم ما كنتم تزعمون ٩٤
وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَٰدَىٰ كَمَا خَلَقْنَـٰكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍۢ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَـٰكُمْ وَرَآءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَـٰٓؤُا۟ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ٩٤
وَلَقَدۡ
جِئۡتُمُونَا
فُرَٰدَىٰ
كَمَا
خَلَقۡنَٰكُمۡ
أَوَّلَ
مَرَّةٖ
وَتَرَكۡتُم
مَّا
خَوَّلۡنَٰكُمۡ
وَرَآءَ
ظُهُورِكُمۡۖ
وَمَا
نَرَىٰ
مَعَكُمۡ
شُفَعَآءَكُمُ
ٱلَّذِينَ
زَعَمۡتُمۡ
أَنَّهُمۡ
فِيكُمۡ
شُرَكَٰٓؤُاْۚ
لَقَد
تَّقَطَّعَ
بَيۡنَكُمۡ
وَضَلَّ
عَنكُم
مَّا
كُنتُمۡ
تَزۡعُمُونَ
٩٤
Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika mumetujia ili muhesabiwe na mulipwe mkiwa peke yenu, kama tulivyowafanya mpatikane ulimwenguni mara ya kwanza mkiwa miguu mitupu, hamuna nguo, mumeviacha nyuma yenu vitu ambavyo tuliwamakinisha navyo miongoni mwa mali ya ulimwenguni mliokuwa mkijigamba nayo. Na hatuwaoni masanamu wako na nyinyi Akhera ambao mlikuwa mkiitakidi kuwa watawaombea na mkidai kuwa ni washirika pamoja na Mwenyezi Mungu katika ibada. Mashikamano yaliyokuwa kati yenu ulimenguni yameondoka, na yamewaondokea yale mliokuwa mkiyadai kwamba waungu wenu ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, na imefunuka wazi kwamba nyinyi ndio mliopata hasara ya nafsi zenu, watu wenu na mali yenu.