Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:95

6:95
۞ ان الله فالق الحب والنوى يخرج الحي من الميت ومخرج الميت من الحي ذالكم الله فانى توفكون ٩٥
۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلْحَبِّ وَٱلنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ ٱلْمَيِّتِ مِنَ ٱلْحَىِّ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ٩٥
۞ إِنَّ
ٱللَّهَ
فَالِقُ
ٱلۡحَبِّ
وَٱلنَّوَىٰۖ
يُخۡرِجُ
ٱلۡحَيَّ
مِنَ
ٱلۡمَيِّتِ
وَمُخۡرِجُ
ٱلۡمَيِّتِ
مِنَ
ٱلۡحَيِّۚ
ذَٰلِكُمُ
ٱللَّهُۖ
فَأَنَّىٰ
تُؤۡفَكُونَ
٩٥
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anapasua mbegu ukatoka mmea, na Anapasua koko ukatoka mti. Anatoa chenye uhai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu na mnyama kutokana na tone la manii ya binadamu na mnyama. Na Anatoa kilichokufa kutokana na chenye uhai, kama tone la manii linalotokana na binadamu na mnyama. Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu. Yaani Mwenye kufanya hili ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika, Anayestahiki kuabudiwa. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na haki mpelekwe kwenye batili mkamuabudu pamoja na Yeye mwingine asiyekuwa Yeye?