Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Siku ambayo tutaikunja mbingu kame vile ukurasa unaokunjiwa maandishi yaliyomo ndani na tutawafufua viumbe kama vile walivyokuwa mwanzo walipozaliwa na mama zao. Hiyo ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyokwenda kinyume. Tumeliahidi hilo ahadi ya kweli tuliyojilazimisha nayo. Hakika sisi daima ni wenye kufanya tunaloahidi.