Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa hakika, tuliandika kwenye vitabu vilivyoteremshwa, baada ya kuwa yashaandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa, kwamba ardhi watairithi waja wa Mwenyezi Mungu walio wema, wale wanaosimama imara kwa yale waliyoamrishwa na wakajiepusha na yale waliyokatazwa, nao ni ummah wa Muhammad, rehema na amani ya Mwenyezi Mungu zishukiye.