Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana na Arrahmani Mwingi wa Rehema? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaoifanyia haraka adhabu, «Hakuna anayewahifadhi na kuwalinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwashukia , usiku wenu au mchana wenu, katika kulala kwenu au kuangaza kwenu?» Bali wao wamepumbaa na wameghafilika na Qur’ani na mawaidha.