Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mkumbuke Nūḥ, ewe Mtume, alipomuita Mola Wake kabla yako na kabla ya Ibrāhīm na Lūṭ, tukaitika mwito wake na tukamuokoa, yeye na watu wake waliomuamini, na makero makubwa.