Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anbiyaa 21:89

21:89
وزكريا اذ نادى ربه رب لا تذرني فردا وانت خير الوارثين ٨٩
وَزَكَرِيَّآ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرْنِى فَرْدًۭا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْوَٰرِثِينَ ٨٩
وَزَكَرِيَّآ
إِذۡ
نَادَىٰ
رَبَّهُۥ
رَبِّ
لَا
تَذَرۡنِي
فَرۡدٗا
وَأَنتَ
خَيۡرُ
ٱلۡوَٰرِثِينَ
٨٩
Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka, ewe Mtume, kisa cha mja wa Mwenyezi Mungu Zakariyya alipomuomba Mola wake Amtunukie wana, wakati umri wake ulipokuwa mkubwa, kwa kusema, «Mola wangu! Usiniache pweke ni siwe na mwana! Basi nitunuku mrithi wa kusimamia mambo ya Dini kwa watu baada yangu mimi, na wewe Ndiye bora wa wenye kusalia na bora wa wenye kusimamia mambo yangu baada yangu kwa uzuri!»