Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Manabii hawa wote, dini yao ni moja, nayo ni Uislamu. Nao ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kwa kuwa mtiifu na kumpwekesha Yeye kwa ibada. Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Bwana wa viumbe, basi muabuduni, enyi watu, Peke Yake, Asiye na mshirika.