Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Lakini watu walitafautiana juu ya Mitume wao, na wengi wa wafauasi wao katika dini walipambanukana wakawa ni makundi na mapote, wakaabudu viumbe na matamanio. Na wote hao ni wenye kurejea kwetu na ni wenye kuhesabiwa juu ya yale waliyoyafanya.