Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Lau hawa ambao mliwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka walikuwa ni waungu wanaostahiki kuabudiwa, hawangaliingia moto wa Jahanamu pamoja na nyinyi, enyi washirikina. Kwa hakika, wote hao, waabudu na waabudiwa, ni wenye kukaa milele ndani ya moto wa Jahanamu.