Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anfal 8:1

8:1
يسالونك عن الانفال قل الانفال لله والرسول فاتقوا الله واصلحوا ذات بينكم واطيعوا الله ورسوله ان كنتم مومنين ١
يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْأَنفَالِ ۖ قُلِ ٱلْأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَصْلِحُوا۟ ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ١
يَسۡـَٔلُونَكَ
عَنِ
ٱلۡأَنفَالِۖ
قُلِ
ٱلۡأَنفَالُ
لِلَّهِ
وَٱلرَّسُولِۖ
فَٱتَّقُواْ
ٱللَّهَ
وَأَصۡلِحُواْ
ذَاتَ
بَيۡنِكُمۡۖ
وَأَطِيعُواْ
ٱللَّهَ
وَرَسُولَهُۥٓ
إِن
كُنتُم
مُّؤۡمِنِينَ
١
Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Masahaba Zako wanakuuliza, ewe Nabii, kuhusu ngawira siku ya Badr: utawagawia vipi? Waambie, «Jambo lake limeachiwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake» Mtume ndiye mwenye kusimamia ugawaji wake kwa amri ya Mola wake. Basi jikingeni na mateso ya Mwenyezi Mungu wala msithubutu kumuasi, na muache kubishana na kuteta kwa sababu ya mali, na mzitengeneze hali zenu, na mjilazimishe utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake iwapo nyinyi ni Waumini, kwani Imani inapelekea kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.