Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anfal 8:11

8:11
اذ يغشيكم النعاس امنة منه وينزل عليكم من السماء ماء ليطهركم به ويذهب عنكم رجز الشيطان وليربط على قلوبكم ويثبت به الاقدام ١١
إِذْ يُغَشِّيكُمُ ٱلنُّعَاسَ أَمَنَةًۭ مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءًۭ لِّيُطَهِّرَكُم بِهِۦ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ ٱلشَّيْطَـٰنِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ ٱلْأَقْدَامَ ١١
إِذۡ
يُغَشِّيكُمُ
ٱلنُّعَاسَ
أَمَنَةٗ
مِّنۡهُ
وَيُنَزِّلُ
عَلَيۡكُم
مِّنَ
ٱلسَّمَآءِ
مَآءٗ
لِّيُطَهِّرَكُم
بِهِۦ
وَيُذۡهِبَ
عَنكُمۡ
رِجۡزَ
ٱلشَّيۡطَٰنِ
وَلِيَرۡبِطَ
عَلَىٰ
قُلُوبِكُمۡ
وَيُثَبِّتَ
بِهِ
ٱلۡأَقۡدَامَ
١١
Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shet'ani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu yenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kumbukeni pindi Mwenyezi Mungu Alipowatia usingizi, ili kuwapa hisia ya amani ya kutoogopa kwamba adui yenu atawashinda, na kuwateremshia kutoka mawinguni maji safi, ili mjisafishe kwayo na uchafu wa nje na Awaondolee, ndani, wasiwasi na mawazo yanayoletwa na Shetani, na ili Aziimarishe nyoyo zenu kwa kuvumilia kwenye vita, na ili nyayo za Waumini ziwe thabiti zisiteleze kwa kuifanya ngumu ardhi ya mchanga kwa mvua hiyo.