Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakukuwa kuswali kwao kwenye Msikiti wa H(arām isipokuwa ni kupiga mbinja na kupiga makofi, basi onjeni adhabu ya kuuawa na kutekwa siku ya Badr kwa sababu ya kukanusha kwenu na vitendo vyenu ambavyo hakuna mwenye kujitokeza kuvitenda isipokuwa makafiri wenye kukataa upweke wa Mola wao na utume wa Nabii wao.