Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anfal 8:43

8:43
اذ يريكهم الله في منامك قليلا ولو اراكهم كثيرا لفشلتم ولتنازعتم في الامر ولاكن الله سلم انه عليم بذات الصدور ٤٣
إِذْ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِى مَنَامِكَ قَلِيلًۭا ۖ وَلَوْ أَرَىٰكَهُمْ كَثِيرًۭا لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَـٰزَعْتُمْ فِى ٱلْأَمْرِ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَ ۗ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ٤٣
إِذۡ
يُرِيكَهُمُ
ٱللَّهُ
فِي
مَنَامِكَ
قَلِيلٗاۖ
وَلَوۡ
أَرَىٰكَهُمۡ
كَثِيرٗا
لَّفَشِلۡتُمۡ
وَلَتَنَٰزَعۡتُمۡ
فِي
ٱلۡأَمۡرِ
وَلَٰكِنَّ
ٱللَّهَ
سَلَّمَۚ
إِنَّهُۥ
عَلِيمُۢ
بِذَاتِ
ٱلصُّدُورِ
٤٣
Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache - na lau angeli kuonyesha kuwa ni wengi, mngeli ingiwa na woga, na mngeli zozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu kakuvueni. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua yalio vifuani. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka, ewe Nabii, pindi Mwenyezi Mungu Alipokuonyesha uchache wa maadui zako ukiwa usingizini na ukawajulisha Waumini kuhusu hilo, ndipo nyoyo zao zikapata nguvu na wakawa na ujasiri wa kupigana nao. Na kama Anagalikuonyesha Mola wako wingi wa maadui zako, basi wangalisita Maswahaba wako kupambana nao, na mungalipatwa na uoga na mkatafautiana kuhusu kupigana, lakini Mwenyezi Mungu Aliepusha jambo la nyinyi kushindwa na Akaokoa na mwisho mbaya wa hilo. Hakika Yeye ni Mjuzi mno wa yaliyofichika nyoyoni na maumbile ya nafsi.