Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono yenu, na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Malipo hayo ambayo yamewapata nyinyi, enyi washirikina, ni kwa sababu ya matendo yenu maovu katika maisha yenu ya duniani. Na Mwenyezi Mungu hamdhulumu yoyote, kati ya viumbe Wake, kitu chochote hata kadiri ya uzito wa chungu mdogo. Bali Yeye Ndiye Mwamuzi Muadilifu Asiyedhulumu.