Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Anfal 8:70

8:70
يا ايها النبي قل لمن في ايديكم من الاسرى ان يعلم الله في قلوبكم خيرا يوتكم خيرا مما اخذ منكم ويغفر لكم والله غفور رحيم ٧٠
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ قُل لِّمَن فِىٓ أَيْدِيكُم مِّنَ ٱلْأَسْرَىٰٓ إِن يَعْلَمِ ٱللَّهُ فِى قُلُوبِكُمْ خَيْرًۭا يُؤْتِكُمْ خَيْرًۭا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌۭ رَّحِيمٌۭ ٧٠
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلنَّبِيُّ
قُل
لِّمَن
فِيٓ
أَيۡدِيكُم
مِّنَ
ٱلۡأَسۡرَىٰٓ
إِن
يَعۡلَمِ
ٱللَّهُ
فِي
قُلُوبِكُمۡ
خَيۡرٗا
يُؤۡتِكُمۡ
خَيۡرٗا
مِّمَّآ
أُخِذَ
مِنكُمۡ
وَيَغۡفِرۡ
لَكُمۡۚ
وَٱللَّهُ
غَفُورٞ
رَّحِيمٞ
٧٠
Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi akiona kheri yoyote nyoyoni mwenu atakupeni bora kuliko vilivyo chukuliwa kwenu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ewe Nabii, waambie mliowateka siku ya vita vya Badr, «Msisikitike juu ya fidia iliyochukuliwa kutoka kwenu. Iwapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Atajua kwamba kwenye nyoyo zenu pana wema, basi Atawapa kilicho bora zaidi kuliko mali yaliyochukuliwa kutoka kwenu, kwa kuwarahisishia nyinyi, kwa hisani Yake, wema mwingi - Mwenyezi Mungu Alitekeleza ahadi Yake kwa 'Abbas, Mwenyezi Mungu Awe radhi naye, na wengineo- na Atawasamehe madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha wa madhambi ya waja Wake wanapotubia, ni Mwenye huruma kwao.