Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati Ibrāhīm na Ismāīl walipoinua misingi ya Alkaba, huku wakimuomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, “Ewe Mola wetu! Tutakabalie amali zetu njema na dua zetu! Kwani wewe Ndiye mwenye kusikia maneno ya waja wako, Ndiye mwenye kujua hali zao.