Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Ibrāhīm na Ya’qūb waliwahimiza watoto wao kusimama imara juu ya Uislamu wakiwaambia, “Enyi watoto wetu! Mwenyezi Mungu Amewachagulia Dini hii, nayo ni Uislamu, Msiiache muda wa uhai wenu, na msifikiwe na mauti isipokuwa na nyinyi muko kwenye Dini hii.”