ان الذين يكتمون ما انزل الله من الكتاب ويشترون به ثمنا قليلا اولايك ما ياكلون في بطونهم الا النار ولا يكلمهم الله يوم القيامة ولا يزكيهم ولهم عذاب اليم ١٧٤
Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa moto, wala Mwenyezi Mungu hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao watapata adhabu chungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika wale wafichao yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika vitabu vyake miongoni mwa sifa za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na mengineyo ya haki na wakawa na pupa la kuchukua badali ndogo ya pambo la maisha ya duniani kama malipo ya kuficha hayo. Hawa hawakili kile wakilacho kwa kuficha haki isipokuwa moto wa Jahanamu utakaokuwa ukiwaka kwa ukali katika matumbo yao. Wala Mwenyezi Mungu Hatasema nao Siku ya Kiyama kwa hasira Zake na machukivu Yake juu yao, wala Hatawatakasa na uchafu wa madhambi yao na ukafiri wao, na itawapata adhabu iumizayo.