Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha: hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na iwe kuondoka kwenu kutoka kisimamo cha Arafa, ambapo ndipo alipoondoka Ibrahim, amani imshukie, ni katika hali ya kumkhalifu, kwa hilo, yule asiyesimama hapo miongoni mwa watu wa zama za ujinga. Na muombeni Mwenyezi Mungu Awasamehe madhambi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaghufiria waja wake waombao maghufira, wanaotubia, ni mwenye huruma kwao.