Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Waumini wa ummah huu waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake na wakatekeleza Sheria Yake, na wale waliokuwa kabla ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa ummah waliopita katika Mayahudi, Wanaswara na Wasabai (Sābiūn), nao ni watu walioko kwenye tabia za maumbile na hawana dini maalumu wanayoifuata, wote hawa wakimuamini Mwenyezi Mungu, imani ya sawa iliyotakasika, wakaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo na wakafanya amali zenye kumridhi Mwenyezi Mungu, basi thawabu zao zimethibiti kwa Mola wao. Wao hawatakuwa na khofu juu ya mambo yao ya Akhera ambayo wao watayakabili. Na wala wao hawatahuzunika juu ya mambo ya dunia waliyoyakosa. Ama baada ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, kuwa ni mwisho wa Manabii na Mitume, kwa watu wote, Mwenyezi Mungu Hatakubali dini, kwa yoyote, isipokuwa ile aliyokuja nayo ambayo ni Uislamu.