Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake, mngeli kuwa miongoni mwa wenye kukhasirika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kisha mlienda kinyume na mkaasi mara nyingine, baada ya kuchukuwa ahadi ya mkazo na kunyanyuliwa jabali, kama desturi yenu daima. Na lau si wema wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake kuikubali toba yenu na kuyasamehe makosa yenu, mungalikuwa ni wenye hasara ya duniani na ya Akhera.