Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo Ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Tukasema, “Mpigeni aliyeuliwa kwa sehemu ya yule ng’ombe aliyechinjwa, Mwenyezi Mungu atamfufua akiwa hai na atawaambia muuaji wake ni nani.” Basi wakampiga kwa ile sehemu ya ng’ombe, Mwenyezi Mungu Akamhuisha na akamtaja muuaji wake. Hivyo ndivyo Anavyohuisha Mwenyezi Mungu wafu Siku ya Kiyama na kuwaonyesha nyinyi, Wana wa Isrāīl, miujiza Yake yenye dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ili mfikiri kwa akili zenu mpate kujiepusha na vitendo vya kumuasi.