Na tulipo chukua agano lenu kuwa hamtamwaga damu zenu, wala hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali nanyi mnashuhudia. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, tulipochukua kwenu ahadi ya mkazo katika Taurati ya kuharamisha umwagaji damu baina yenu, nyinyi kwa nyinyi, na kutoana majumbani nyinyi kwa nyinyi. Kisha mkakubali hilo na hali nyinyi mnashuhudia kuwa ni kweli.