Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:89

2:89
ولما جاءهم كتاب من عند الله مصدق لما معهم وكانوا من قبل يستفتحون على الذين كفروا فلما جاءهم ما عرفوا كفروا به فلعنة الله على الكافرين ٨٩
وَلَمَّا جَآءَهُمْ كِتَـٰبٌۭ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٌۭ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا۟ مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُوا۟ كَفَرُوا۟ بِهِۦ ۚ فَلَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ ٨٩
وَلَمَّا
جَآءَهُمۡ
كِتَٰبٞ
مِّنۡ
عِندِ
ٱللَّهِ
مُصَدِّقٞ
لِّمَا
مَعَهُمۡ
وَكَانُواْ
مِن
قَبۡلُ
يَسۡتَفۡتِحُونَ
عَلَى
ٱلَّذِينَ
كَفَرُواْ
فَلَمَّا
جَآءَهُم
مَّا
عَرَفُواْ
كَفَرُواْ
بِهِۦۚ
فَلَعۡنَةُ
ٱللَّهِ
عَلَى
ٱلۡكَٰفِرِينَ
٨٩
Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na ilipowajia Qur’ani inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, ikisadikisha yale ambayo waliokuwa nayo kwenye Taurati, waliikanusha na kuukataa utume wa Muhammad, rehema na mani zimshukie. Na walikuwa, kabla ya kutumilizwa kwake, wakitumai kusaidiwa na yeye dhidhi ya washirikina wa Kiarabu, na walikuwa wakisema, “Umekaribia wakati wa kutumilizwa Mtume wa zama za mwisho ambaye sisi tutamfuata na tutapigana na nyinyi tukiwa pamoja na yeye.” Alipowajia huyo Mtume, ambaye walizijua sifa zake na ukweli wake, walimkataa na walimkanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu imshukie kila aliyemkanusha Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema na amani zimshukie, na kukanusha Kitabu chake ambacho Mwenyezi Mungu alimletea kwa njia ya Wahyi.