Na kwa yakini wao wanafika kwenye nchi ilio teremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiiona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na washirikina wa Makkah walikuwa wakikipitia kijiji cha watu wa Lūṭ katika safari zao, nacho ni kijiji cha Sadūm ambacho kiliangamizwa kwa mawe kutoka mbinguni, wasizingatie kwa hilo, bali walikuwa hawatazamii kuwa kuna marejeo Siku ya Kiyama ambapo wao watalipwa.