Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapate kukumbuka. Lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na hakika tunateremsha mvua juu ya sehemu ya ardhi bila ya nyingine, ili wale walioteremshiwa mvua wapate kukumbuka neema ya Mwenyezi Mungu juu yao na wamshukuru, na ili wale walionyimwa mvua wafanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Apate kuwarehemu wao na kuwanywesha. Lakini wengi wa watu wanakataa isipokuwa ni kukanusha neema zetu juu yao, kama neno lao wanalolisema, «tumeletewa mvua kwa sababu ya nyota kadha na kadha.»