Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyo wafaa wala yasiyo wadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na pamoja na dalili hizi za uweza wa Mwenyezi Mungu na wema Wake kwa viumbe Wake, makafiri wanaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, kitu ambacho hakiwanufaishi wakikiabudu wala hakiwadhuru wakiacha kukiabudu. Na kafiri ni msaidizi wa Shetani juu ya Mola wake, kwa kufanya ushirikina katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na ni mwenye kumpa nguvu huyo Shetani juu kumuasi Mwenyezi Mungu.