Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kisha wale mahujaji wakamilishe matendo ya ibada yaliyosalia ya kujifungua na kutoka kwenye kifungo cha ibada yao ya Hija, nako ni kwa kuondoa uchafu uliokusanyika kwenye miili yao, kukata kucha zao na kunyoa nywele zao, na watekeleze yale waliyojilazimsha nafsi zao ya kuhiji na kufanya Umra na kuchinja wanyama wa tunu, na waitufu kwa kuizunguka Nyumba huru ya kale ambayo Mwenyezi Mungu Ameikomboa isitawaliwe kimabavu na watu wasioijali, nayo ni Alkaba.