Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hajj 22:30

22:30
ذالك ومن يعظم حرمات الله فهو خير له عند ربه واحلت لكم الانعام الا ما يتلى عليكم فاجتنبوا الرجس من الاوثان واجتنبوا قول الزور ٣٠
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَـٰتِ ٱللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌۭ لَّهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ ۗ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ ٱلْأَنْعَـٰمُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ ۖ فَٱجْتَنِبُوا۟ ٱلرِّجْسَ مِنَ ٱلْأَوْثَـٰنِ وَٱجْتَنِبُوا۟ قَوْلَ ٱلزُّورِ ٣٠
ذَٰلِكَۖ
وَمَن
يُعَظِّمۡ
حُرُمَٰتِ
ٱللَّهِ
فَهُوَ
خَيۡرٞ
لَّهُۥ
عِندَ
رَبِّهِۦۗ
وَأُحِلَّتۡ
لَكُمُ
ٱلۡأَنۡعَٰمُ
إِلَّا
مَا
يُتۡلَىٰ
عَلَيۡكُمۡۖ
فَٱجۡتَنِبُواْ
ٱلرِّجۡسَ
مِنَ
ٱلۡأَوۡثَٰنِ
وَٱجۡتَنِبُواْ
قَوۡلَ
ٱلزُّورِ
٣٠
Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi. Na mmehalalishiwa nyama hoa ila wale mlio somewa. Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uwongo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hiyo Aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ya kuondoa uchafu, kutekeleza nadhiri na kuitufu Nyumba ndiyo Aliyoyapasisha Mwenyezi Mungu, basi yatukuzeni. Na yoyote mwenye kuyatukuza Aliyoyatakasa Mwenyezi Mungu, na miongoni mwayo ni matendo Aliyoyawekea ibada ya Hija kwa kuyatekeleza kikamilifu kwa kumtakasia Mwenyezi Mungu, basi hilo ni bora zaidi kwake, ulimwenguni na Akhera. Na Mwenyezi Mungu Amewahalalishia nyinyi kula wanyama-howa isipokuwa kile Alichokiharamisha kwenu katika kile mnachosomewa ndani ya Qur’ani miongoni mwa mizoga na mengineyo, basi kiepukeni. Katika hili pana kubatilisha kile ambacho Waarabu walikuwa wakikiharamisha cha baadhi ya wanyama-howa. Na jiekeni mbali na uchafu ambao ni masanamu na urongo wa kumzulia Mwenyezi Mungu.