Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hajj 22:37

22:37
لن ينال الله لحومها ولا دماوها ولاكن يناله التقوى منكم كذالك سخرها لكم لتكبروا الله على ما هداكم وبشر المحسنين ٣٧
لَن يَنَالَ ٱللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَآؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ ٱلتَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُحْسِنِينَ ٣٧
لَن
يَنَالَ
ٱللَّهَ
لُحُومُهَا
وَلَا
دِمَآؤُهَا
وَلَٰكِن
يَنَالُهُ
ٱلتَّقۡوَىٰ
مِنكُمۡۚ
كَذَٰلِكَ
سَخَّرَهَا
لَكُمۡ
لِتُكَبِّرُواْ
ٱللَّهَ
عَلَىٰ
مَا
هَدَىٰكُمۡۗ
وَبَشِّرِ
ٱلۡمُحۡسِنِينَ
٣٧
Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hazitamfikia Mwenyezi Mungu nyama za vichinjwa hivyi wala damu zake kitu chochote, kitakachomfikia Yeye ni kule kumtakasia kwenu katika hivyo na kuwa lengo lake ni radhi za Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hivyo basi Amewadhalilishia nyinyi, enyi wenye kujikurubisha, ili mumtukuze Mwenyezi Mungu na mumshukuru kwa kuwaongoza kwenye haki, kwani Yeye Anastahiki hilo. Na uwape bishara njema, ewe Nabii, wenye kufanya wema kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake na kuwafanyia wema viumbe vyake, kupata kila lema na kufaulu.