Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hajj 22:60

22:60
۞ ذالك ومن عاقب بمثل ما عوقب به ثم بغي عليه لينصرنه الله ان الله لعفو غفور ٦٠
۞ ذَٰلِكَ وَمَنْ عَاقَبَ بِمِثْلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِىَ عَلَيْهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌۭ ٦٠
۞ ذَٰلِكَۖ
وَمَنۡ
عَاقَبَ
بِمِثۡلِ
مَا
عُوقِبَ
بِهِۦ
ثُمَّ
بُغِيَ
عَلَيۡهِ
لَيَنصُرَنَّهُ
ٱللَّهُۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
لَعَفُوٌّ
غَفُورٞ
٦٠
Ndio namna hivi. Na anaye lipiza mfano wa alivyo adhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye maghfira. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hilo ni jambo tulilokusimulia la kuwatia Peponi waliogura(katika njia ya Mwenyezi Mungu), na mwenye kufanyiwa uadui na kuonewa basi yeye ameruhusiwa kupambana na huyo mhalifu kwa kitendo kama chake, na atakuwa hana makosa. Na akirudi yule mhalifu kumuonea na akafanya udhalimu, basi Mwenyezi Mungu Atampa ushindi yule mdhulumiwa aliyeonewa, kwani haifai afanyiwe uadui kwa kuwa amejilipizia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehefu ni Mwingi wa kughofiria, Anasamehe dhambi za wenye kukosea, hawafanyii haraka kuwatesa na anazifinika dhambi zao.