Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hajj 22:65

22:65
الم تر ان الله سخر لكم ما في الارض والفلك تجري في البحر بامره ويمسك السماء ان تقع على الارض الا باذنه ان الله بالناس لرءوف رحيم ٦٥
أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ وَٱلْفُلْكَ تَجْرِى فِى ٱلْبَحْرِ بِأَمْرِهِۦ وَيُمْسِكُ ٱلسَّمَآءَ أَن تَقَعَ عَلَى ٱلْأَرْضِ إِلَّا بِإِذْنِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٌۭ رَّحِيمٌۭ ٦٥
أَلَمۡ
تَرَ
أَنَّ
ٱللَّهَ
سَخَّرَ
لَكُم
مَّا
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
وَٱلۡفُلۡكَ
تَجۡرِي
فِي
ٱلۡبَحۡرِ
بِأَمۡرِهِۦ
وَيُمۡسِكُ
ٱلسَّمَآءَ
أَن
تَقَعَ
عَلَى
ٱلۡأَرۡضِ
إِلَّا
بِإِذۡنِهِۦٓۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
بِٱلنَّاسِ
لَرَءُوفٞ
رَّحِيمٞ
٦٥
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu amevidhalilisha kwenu viliomo katika ardhi, na marikebu zipitazo baharini kwa amri yake, na amezishika mbingu zisianguke juu ya ardhi ila kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma kwa watu, Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewadhalilishia vilivyoko ardhini miongoni mwa vitu vitambaavyo na wanyama na nafaka na matunda na vitu visivyo na roho, kwa ajili ya kipando chenu, chakula chenu na manufaa yenu, kama Alivyowadhalilishia mashua zinazotembea baharini kwa uweza Wake na amri Yake, ziwabebe nyinyi na vyombo vyenu ziwafikishe kwenye miji na sehemu mzitakazo na kwamba Yeye Ndiye Anayeizuia mbingu na kuitunza, ili isianguke juu ya ardhi ikawaangamiza walioko juu yake isipokuwa kwa idhini Yake, Aliyetakasika na kila sifa za upungufu, kuwa hilo lifanyike, ili Awarehemu watu rehema kunjufu katika mambo yao ya hivi sasa hapa duniani na ya baadaye kesho Akhera? Na miongoni mwa rehema Zake ni vitu hivi Alivowadhalilishia na vinginevyo kwa fadhila Zake juu yao.